Wana Ukoo niwaletee salamu za upendo.
Leo hii Ntemi Makwaia III, wa XXIII wa Busiya hapa Dodoma nimefanya kikao na Afisa Mwandamizi kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani kwa lengo la kurasimisha Utemi wetu wa Busiya, tutambulike kisheria na kuzilinda rasilimali zetu yakiwemo mashamba na mali kale zetu zote. Wizara imetupa miongozo na mchakato huu utaanza mara moja.
Ntemi Makwaia III, wa XXIII wa Busiya.


